BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

MIONGONI MWA HEKIMA ZA IMAMU ALI BIN ABITALIB (A.S)

ULEVI WA UJANA

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema:

 "Ujana ni matawi ya uendawazimu."[1] Imam Ali (a.s.) amesema: "Aina za ulevi ni nne: Ulevi wa ujana, ulevi wa mali, ulevu wa kulala na ulevi wa ufalme."[2]

Imam Ali (a.s.) amesema: "Inapasa kwa mwenye akili ajiepushe na ulevi wa mali, ulevi wa uwezo, ulevi wa elimu, ulevi wa sifa, na ulevi wa ujana, kwani hakika hayo yote yana riha mbaya inayoondoa akili na kupunguza unyenyekevu."[3]

 Imepokewa kuwa Imam Ali na Maimamu (a.s.) walikuwa wakiomba ndani ya mwezi wa Shabani: "Ewe Mungu wangu nimemaliza umri wangu kwenye shari ya kukusahau Wewe. Na nimeumaliza ujana wangu katika ulevi wa kujitenga na Wewe. Ewe Mungu wangu ni siku nyingi sijaamka kwa ajili ya kukufanyia ujeuri, na kurakibu nikielekea njia ya ghadhabu Yako."[4]

MATAMANIO YA KIJINSIA

Mtego wa Shetani:

Mwenyezi Mungu amesema:

قُل لِّلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ اَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ذٰلِكَ اَزْكَي لَهُمْ إِنَّ اللهَ خَبِيرٌ بِمَا يَصْنَعُونَ1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next