BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

MAELEZO YA IMAMU ALIY (A.S) KUHUSIANA NA UADILIFU

Uadilifu hautakiwi kuwekwa kando kwa sababu ya kughilibika na manufaa au tamaa na mali za dunia.

Hivi leo ubaguzi, kuteuana na kupeana kazi kijamaa, kubwagia tonge kubwa kubwa za rushwa, ndio mambo yalioenea idarani mwote, na mambo hayo yamegeuzwa kua ni moja yati ya nyenzo za kisiasa na kuendesha nchi katika jamii, lakini unahodha wa jahazi ya kisiasa ulipomfikia Ali (a.s) hayanyamazia mambo hayo na badala yake Yeye alikua ni adui wa mambo kama hayo, lengo lake lilikua ni kupiga vita siasa za aina kama hiyo, hilo ndilo lililowafanya wanyonyaji walioko serekalini kukasirika na kuto ridhika na uongozi wake, na hicho ndicho kikawa chanzo cha fitina katika utawala wake, hapo ndipo baadhi ya marafiki wa Ali (a.s) walipomwendea na kujaribu kumpa mawazo na kumwambia:

“kwa kutokana na maslahi yako na usalama wako, basi waonaje  kama utaachilia mbali suala la kuweka haki sawa katika jamii, hasa hasa ukizingatia kua wenye kulipinga suala hili ni miongoni mwa Masahaba ambao ni maaadui wako, huku ukizingatia kua baadhi ya maadui hao wameshika madaraka ktika sehemu zilizo muhimu, kama vile Muaawiya aliyeshika madaraka katika mji wa Shaam.

Basi jiepushe na matatizo kwa kutoyaingilia masuala yao na dhulma wanazozifanya”.

 Ali (a.s) aliwajibu kwa kusema:

“hivi mnanitaka nijitafutie ushindi na madaraka kwa kupitia dhulma? Mnanitaka mimi niuchinje uadilifu kwa kupitia kisu cha siasa? Naapa kwa kwa Mwenye Enzi Mungu kua, mimi sitoyafuata mawazo yenu, bali nitashikamana na uadilifu, na hata kama ingalikua mali hii iliokuwepo katika benki ya Waislamu ni mali yangu binafsi, basi nisingelibagua katika ugaeaji wa mali hiyo katika jamii bali ningaliigawa mali hiyo kwa usawa, basi vipi mimi leo nifanye ubaguzi katika mali ya Mwenye Enzi Mungu iliowekwa amana kwangu name si mmiliki wa mali hiyo.

Hivi ndivyo Ali (a.s) anavyo yafanyia tathmini anayopewa kabla ya kuyafanyia kazi na hivi ndivyo Yeye anavyoitathmini jamii.

 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 next