UGAIDI
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

MWELEKEO KATIKA KUTAFSIRI UGAIDI (TERRORISM)


Makala haya yameandikwa na:
Shaykh Muhammad 'Ali Taskhiri

Yametarjumiwa na:
Amiraly M.H. Datoo (PO Box 838 Bukoba, Tanzania)

PANDE MBILI ZINAPO PINGANA, KILA MMOJA HUMWITA MWENZAKE KUWA NI MGAIDI.

SASA JE MGAIDI NI NANI BAINA YAO ? TUSOME...

Azimio 20/5 - (I.S) la Mkutano Mkuu wa tano uliunga mkono wazo la kuitisha Baraza la Kimataifa chini ya Umoja wa Mataifa ili kuzungumzia swala la ugaidi wa kimataifa na kuweza kufafanua na kutofautisha baina ya harakati za wananchi kwa kutambua haki zao za kitaifa na ule ukombozi wa ardhi zao.

Hivyo inamaanisha kuwa sisi, katika kikao hiki tuzingatie hatua zifuatazo:

  • Turejee kwanza kabisa katika vianzo vya Islam ili kutengeneza hoja madhubuti, kutambulisha misingi kwa mujibu wa malengo na matendo ya kibinadamu yakadiriwavyo, na kubuni misingi juu ya uamuzi wetu katika masuala mbalimbali.
  • Kuchunguza hali halisi ya maumbile ya binadamu yasiyokuwa na tuhuma yoyote ili kuweza kutambulisha hukumu za kibinadamu zinazoweza kuletwa mbele ya jumuiya ya Kimatafa zikiwa ni kama misingi ya kibinadamu ya kupambanua. Kwa ajili ya haya, matokeo ya masomo yetu lazima yazingatie nyanja mbalimbali za mtazamo wa Kimataifa na kutoa mpangilio wa utekelezaji kwa ujumla.
  • Kutokana na kanuni hizi za Kiislamu na kibinadamu, sisi tunadadisi ufafanuzi sahihi na aina yake pekee, i.e. ikizungukia sifa zote za ugaidi na kutoa nadharia za kupambanua ugaidi ambapo haiwezekani kukubalika kama ndiyo kanuni nzuri.
  • Hivyo basi, inatubidi kuweka mpambanuo halisi maana na ufafanuzi wa ugaidi mbele ya jumuiya za nchi na kimataifa. Inatubidi kuchunguza kila mojawapo kwa ukaribu katika mwangaza wa matokeo, na hivyo kutoa uamuzi sahihi ambao utakuwa huru bila ya chuki au kupotosha na kulitazama kila jambo kwa malengo sahihi.

Katika mwangaza wa utambulisho huu, mazungumzo yetu yatakuwa yamebakia katika nyanja zifuatazo:

Hoja ya kwanza: Ni dhahiri kuwa kila Taifa, kila Nchi au kwa uhalisi kila Jumuiya inakuwa na wapinzani wake ambayo yanataka kuwatokemeza wapinzani wao, na vile mzozo wao utakavyoendelea kukua basi hugeukia sura ya fujo, kila upande unajaribu kuharibu jina la mpinzani wake kwa tuhuma za kuwaita waasi, majangili, wavunja sheria, matendo yasiyokuwa ya binadamu, magaidi, na majina tele yanayowezekana kutumiwa.

Sisi tunaona kuwa kila upande unajiingiza katika tuhuma kama hizo ili kutekeleza mipango ambayo inauondolea upande wa pili haki kwa masingizio ya kushirikiana pamoja na maadui wao au kufanya njama dhidi ya matakwa yao halali.1 2 3 4 5 6 7 next