Misingi ya diniDeprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 Iko kwenye alhassanain ishawekwa MATAWI YA DINI Kabla ya kuanza kubainisha na kufafanua sehemu ya pili katika mafunzo ya juu ya Uislaam, hapana budi kuashiria hapa ya kuwa sehemu ya kwanza ya mafunzo ya kiislaam ya hali ya juu na yaliyo matukufu yaani: Usulud-dini ambazo tumezi zungumzia, ni lazima mwanadamu aziitakidi au awe na itikadi nazo-kwani misingi hiyo ndio inayo husiana na ukafiri na itikadi- kutokana na ijtihadi na kwa kutegemea dalili na wala haitoshi kwenye misingi hiyo kujitegemeza sehemu fulani au kwa mtu fulani na kumfuata mtu huyo. Wakati ambapo Furuud-dini (matawi ya dini), ambayo hivi sasa tuko mbioni kuyafafanua na kuyazungumzia, hakika matawi hayo yameenea na kuzihusu sehemu na nyanja zote za maisha na yanazihusu harakati zote za mwanadamu na matendo yake yote kabla ya kuzaliwa kwake mpaka baada ya kufariki kwake na maranyingi mwanadam-kwa sababu ni mambo yanayo husiana na matendo kama harakati za mwanadamu na kutulia kwake na utendaji au utekelezaji wa mambo ya aina tofauti na mabadiliko-hawezi kufanya ijtihadi (kujitahihi) katika mambo yote hayo na kufahamu hukumu zake kutokana na dalili zake kwa uchambuzi wake ulio tajwa katika vyanzo vine vya sheria: Qur'ani tukufu, Sunna sharifu- Yaani hadithi za Mtume (s.a.w) na riwaya za Ahlul bayti (a.s)- na Ijmaa (Makubaliano ya wanazuoni) na Akili, kwa hivyo Uislaam ukajuzisha (ukamruhusu) kwa mwanadamu kumfuata mujtahidi alie kusanya masharti ya kufuatwa (kufanyiwa taqliid) kwenye mas'ala hayo na kurejea kwake katika mas'ala hayo kwa ajili ya kumfanyia wepesi na kumrahisishia mambo.
|