KUMJUA MWENYEEZI MUNGUDeprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 SOMO LA KWANZA
QUR-ANI NI KITABU CHA KUMFAHAMU NA KUMJUA MWENYEEZI MUNGU
Kwa kutarajia msaada kutoka kwa Mwenyeezi Mungu tunataka kujifunza na kujua maana ya Aya za Qur-ani, na vipi tutaweza kuzitafsiri na kuziletea maana Aya hizo. Tunataka kufahamu maana ya Aya za Qur-ani ili tuweze kumjua Mwenyeezi Mungu zaidi, Mwenyeezi Mungu ambaye ndiye anayetuongoza sisi katika njia ya uongofu, na amemchagua Mtume wetu Muhammad (s.a.w) ili atufunze sisi kitabu chake hicho cha Qur-ani, na atuonyeshe na kutuongoza njia ambayo ni sahihi itakayotuwezesha kufikia katika saada. Ewe Mola uliye pekee tunakutakasa na kukushukuru kutokana na neema zako kubwa na nyingi ulizotusabilia sisi.
|