ufahamu wa Quran
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

MAELEZO KUHUSIANA NA KITABU HIKI

 

1. Kitabu hiki kimekusanya masomo saba, kila somo lina utangulizi, ibara kumi za Qur-ani, jaduweli mbili za maneno, na aina tatu za tamrini yaani (kazi za nyumbani), na somo la mwisho ni kwa ajili ya kujipatia mafunzo mwenyewe yule anayejifunza ambapo vile vile kuna kazi nyengine zinazomuwajibikia kuzifanya ili kujikumbusha na yale masomo aliyosoma hapo mwanzo.

 

2.  Kila somo lina kazi tatu, kazi ya mwanzo ina masuala ishirini, ambayo ni masuala ya testi za kuchaguwa kwa mfano:-

(a, b, c, d) , kazi ya pili kuna ibara kumi za Qur-ani ambazo zinatakiwa kutarjumiwa na kuandikwa chini yake, katika kazi ya tatu kuna masuala manne ambayo yanatakiwa kujibiwa kwa mtindo wa ibara za Qur-ani, madhumuni au hadafu ya kazi ya tatu ni kuwawezesha wale wanaojifunza Qur-ani kuweza kubainisha mambo ya kiislamu na kujiwekea mawasiliano na itikadi za kidini zilizo sahihi kwa kutumia misingi ya Qur-ani.

 

NJIA AU NYENZO ZA KUFUNDISHIA

 

Kabla ya kuelezea na kufafanua njia za kufundishia Qur-ani hakuna budi kuelezea nukta chache ambazo zina faida ndani yake, hakuna shaka kwamba kila kazi au matendo ambayo mwanaadamu anayatenda katika maisha yake ya kila siku ikiwemo kazi hiyo ya kutoa mafunzo ya Qur-ani ni lazima tuyafanye matendo hayo tukiwa na matumaini ya kutafuta (na kupata) ridhaa ya Mwenyeezi Mungu, kwani kazi au matendo ambayo hufanywa bila ya kupata ridhaa ya Mwenyeezi Mungu huwa sio yenye kudumu yaani (hupotea), ama kazi au matendo ambayo hufanywa kwa ajili ya kutafuta ridhaa ya Mwenyeezi Mungu huwa ni yenye baraka na yenye kudumu na kubaki milele. Mwenyeezi Mungu Mtukufu katika Suratu -An- Nahli anasema:-

 

Mlivyonavyo vitakwisha na vilivyoko kwa Mwenyeezi Mungu (vya jaza yenu) ndivyo vitakavyobakia………..1 2 3 4 5 6 7 8 9 next