METHALI NDANI YA QUR-ANI
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

Ndani ya Qur-ani kumekuja methali za aina tatu. Nazo ni hizi zifuatazo:-

1. Methali iliyokuja kwa kutumiwa nguvu za kiakili, ambazo huweza kumchora au kumuelezea mwanaadamu sifa za nafsi zake. Kiistilaha aina hiyo methali inaitwa mifano, na tumeelezea maudhui yanayohusiana na aina hiyo katika sehemu iliyopita.

2. Methali zinazoelezea kuhusu matokeo ya watu waliopita, matokeo ambayo yana uhakika katika maisha ya mwanaadamu na yametokea kweli, matokeo hayo huleta mafunzo katika jamii ya watu wanaofuata. Mifano ya aina hiyo inaelezea kwa uhakika matokeo yaliyotokea. Kwa mfano katika Suratul-Tahriym Aya ya 10-12 allah (s.w) anasema:-

 

ضَرَبَ اللهُ مَثَلاً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا اِمْرَاَةَ نُوحٍ وَاِمْرَاَةَ لُوطٍ كَانَتَا تَحْتَ عَبْدَيْنِ مِنْ عِبَادِنَا صَالِحَيْنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمَا مِنَ اللهِ شَيْئاً وَقِيلَ ادْخُلاَ النَّارَ مَعَ الدَّاخِلِينَ

 

Mwenyeezi Mungu amepiga (anapiga) mifano wa wale wabaya waliokufuru, ni mkewe Nuhu na Mkewe Luti. Walikuwa chini ya waja wetu wema, wawili hao miongoni mwa waja wetu (wema); lakini (wanawake hao), waliwafanyia hiana (waume zao watukufu hao), na (waume zao hao) hawakuweza kuwasaidia chochote mbele ya Mwenyeezi Mungu na ikasemwa: “Uingieni Moto pamoja na hao wanaouingia.”

 

وَضَرَبَ اللهُ مَثَلاً لِّلَّذِينَ آمَنُوا اِمْرَاَةَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ابْنِ لِى عِندَكَ بَيْتاً فِى الْجَنَّةِ وَنَجِّنِى مِن فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِ وَنَجِّنِى مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 next