NYENZO NA HERUFI ZA VIAPO NDANI YA QUR-ANI
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

NYENZO NA HERUFI ZA VIAPO NDANI YA QUR-ANI

(VITU VILIVYOAPIWA NDANI YA QUR-ANI).

 

Hapo mwanzo tulielezea kuwa kile kitu ambacho kinaapiwa yaani (مقسم به), ni lazima kiwe thabiti ili kulitilia mkazo na kulisisitiza lile jambo ambalo linaapiwa, (مقسم عليه). Wanaadamu huapa kwa kutumia majina ya sifa tukufu za Mwenyeezi Mungu. Yaani (مقسم به), ndani ya Qur-ani kuna vitu vingi vilivyoapiwa na katika sehemu hii tutuvielezea kwa ufupi vitu hivyo. (ili kupata ufafanuzi zaidi rejea kitabu cha Elimu ya Qur-ani, ukurasa wa 305-307).

 

MAJINA YA MWENYEEZI MUNGU YALIYOTUMIKA KWA VIAPO NDANI YA QUR-ANI

 

Majina yaliyotumika kuapia katika Qur-ani ni ya aina mbili, na majina hayo ni katika sifa za dhati za Mwenyeezi Mungu, nayo ni (الله), na (رب), Allah (s.w) katika Suratul-Al-Anaam Aya 23 anasema:-

 

ثُمَّ لَمْ تَكُن فِتْنَتُهُمْ إِلاَّ اَن قَالُواْ وَاللهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ

 

Maana ya Aya hiyo ni kama ifuatavyo:-1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 next