SOMO LA KUMI NA TANO
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

 

SOMO LA KUMI NA TANO
HERUFI MUKATIA

                                                               

Ili kufahamu makusudio yaliyokusudiwa kuhusiana na mada inayoonekana hapo juu, hakuna budi kulifafanua neno (Mukatia) ili lifahamike makusudio (maana) yake.

Herufi Mukatia ni miongoni mwa herufi ishirini na nane ambazo zinatumika katika lugha ya kiarabu, herufi hizo ni hizi zifuatazo:-

(ا,ب,ت,ث,ج,ح,خ,د,ذ,ر,ز,س,ش,ص,ض,ط,ظ,ع,غ,ف,ق,ك,ل,م,ن,و,ه,ي). Herufi Mukatia huandikwa kwa mtindo wa neno kamili, ama husomwa moja moja peke yake, na kwa sababu hiyo basi ndiyo zikaitwa herufi Mukatia.

Moja wapo katika maudhui yaliyozungumzwa ndani ya Qur-ani ni kuhusiana na herufi Mukatia. Katika Qur-ani kuna sura ishirini na tisa ambazo zimeanza na herufi hizo (yaani herufi Mukatia). Kama zitakusanywa herufi hizo ndani ya sura zilizotumika itabainika na kufahamika kuwa kwa ujumla ni herufi 78, ama kama zitafutwa au kuondolewa zile herufi ambazo zinajikariri (zinajirejea) zitabakia herufi kumi na nne, (yaani zitabakia nusu ya herufi hizo za lugha ya kiarabu), kwa sababu herufi zote kwa ujumla (yaani herufi za Kiarabu) ni herufi ishirini na nane. Na ndizo zinazojulikanwa kwa jina la herufi mukatia. Kuna siri kubwa iliyoko kuhusiana na herufi hizo za mukatia, na hakuna mtu yoyote anayeielewa siri hiyo isipokuwa Mwenyeezi Mungu na Mtume wake. Kila herufi miongoni mwa herufi hizo za Mukatia husomwa kwa jina lake la kiarabu. Kwa mfano:-

Neno (المص), neno hilo linasomwa kwa mtindo huu,

 (الف,لام, ميم, صاد).1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 next