SIFA ZA SIMULIZI ZILIZOMO NDANI YA QUR-ANI
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

 

SIFA ZA SIMULIZI ZILIZOMO NDANI YA QUR-ANI

 

Hadithi na simulizi hizo zilizomo ndani ya Qur-ani zina sifa zake, miongoni mwa sifa hizo ni hizi zifuatazo:-

 

1. KUCHAGULIWA KWA SIMULIZI (HADITHI).

 

    Kitabu cha Qur-ani sio kitabu cha tarekh wala historia, bali ni kitabu cha uongofu chenye kuleta muongozo, uongofu, na chenye kuwapa wanaadamu nasaha katika maisha yao ya kila siku.

Kitabu hicho kinaelezea matokeo yote yaliyokuwa muhimu na yasiyokuwa muhimu ambayo yametokea katika kipindi chote cha tarekh, (kwa mfano masuala ya kitabia, tabia njema na tabia mbaya) kwa hiyo katika kunukuu simulizi hizo huchaguliwa kile kipande au sehemu ambayo inatosheleza kufikisha ujumbe, na hakuna hadithi au simulizi yoyote iliyonukuliwa yote kwa ukamilifu, bali huchaguliwa sehemu ambayo ina madhumuni makuu (madhumuni asili), na ni kwa sababu hiyo basi simulizi hizo zilizomo ndani ya Qur-ani zina athari na ujumbe maalumu, tofauti na simulizi, nyengine zinazosimuliwa katika vitabu vyengine, ambazo huangaliwa njia , sababu au watu wanaoinishwa na kuelezewa katika simulizi hizo.

Kwa mfano katika simulizi za Qur-ani kimeelezewa kisa cha As-habul-Kahf (hali ya kuwa hayajatajwa majina ya watu hao), As-habul-fiyl (katika kisa hicho hakujaainishwa majina ya watu wanaohusiana na kisa hicho), ama baadhi ya simulizi zilizomo ndani ya Qur-ani kwa kuzingatia lengo na umuhimu wa mtu ambaye anazungumzwa jina la mtu huyo hutajwa, na kuelezewa sifa zake, kwa mfano (Maryam (a.s)), au huelezewa tokeo la kisa hicho kijumla jamala kwa kuzingatia hadafu na madhumuni ya kisa hicho. Mfano mwengine wa simulizi ambao ni wenye kujalibisha (kutia mori) ni kuhusiana na kisa cha Kaumu  Thamudu, ambacho kimeelezewa katika (Suratul-Shams Aya ya 11-15). Allah (s.w) anasema:-

 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 next