SABABU ZA KUTEREMSHWA QUR_ANI
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

(KITABU MAFUNZO YA ELIMU YA QUR_ANI)

 

Hapana shaka inafahamika na kueleweka ya kwamba Qur-ani imeteremshwa kidogo kidogo kutokana na matokeo masuala au mambo tofauti katika kipindi chote, tangu alipopata utume Nabii Muhammad (s.a.w). Aya nyingi za Qur-ani zimeteremshwa kutokana na matokeo tofauti yaliyokuwa yakitokea katika zama hizo, au ziliteremshwa kutokana na masuala ambayo watu walikuwa wakimuuliza Nabii Muhammad (s.a.w), sababu na sharti hizo zinajulikana kwa jina la ( اسباب نزول) yaani (Sababu za uteremshwaji wa aya za Qur-ani) au (شائن نزول)  yaani (Misingi ya uteremshwaji kwa aya za Qur-ani).

Ni jambo lililowazi na lisiloshaka ndani yake ya kwamba aya za Qur-ani zilizoteremshwa kutokana na kila sababu au mambo tofauti zinalingana na uteremshwaji wake, kwa hiyo pindi itakapokuwa katika aya kuna neno lisilofahamika maana yake au lenye kutatiza kutamkwa kwake, watu wanaweza kulitatua tatizo hilo na kufahamu kwa undani maana ya neno hilo kwa kurejea namna ya uteremshwaji, wakati, sharti au zama iliyoteremshwa aya hiyo, vile vile kutokana na tokeo lililopelekea kuteremshwa kwake, kwa hiyo ili kufahamu maana kamili ya kila aya ni lazima tufahamu na kuelewa sababu za uteremshwaji wa aya za Qur-ani.

Na tutizame mfano wa aya hii ya (Suratul-Al-Baqarah aya ya 158). Allah (s.w) anasema:-

إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَآئِرِ اللهِ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ اَوِ اعْتَمَرَ فَلاَ جُنَاحَ عَلَيْهِ اَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا وَمَن تَطَوَّعَ خَيْراً فَإِنَّ اللّهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ

Maana ya aya hiyo ni kama ifuatavyo:-

“Hakika Safaa na Marwa (Majabali mawili yanayofanyiwa ibada ya kusai huko Makka) ni katika alama au nembo za kuadhimisha dini ya Mwenyeezi Mungu. Basi anayehiji kwenye nyumba hiyo au kufanya Umra, sio kosa kwake kuvizunguka (vilima) hivyo viwili, na anayefanya wema (atalipwa) kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukurani na mjuzi (wa kila jambo)”.

Kuna baadhi ya watu wametowa nadhari zao na kulitilia shaka suala hili ya kwamba, Kusai (alama au nembo) baina ya Majabali hayo mawili ya Safaa na Marwa ni katika nguzo za Hijja na Umra, basi ni kwa nini katika Qur-ani limetumika nenoلاجناح  ? wakati ambapo neno hilo lina maana ya kufanya dhambi?

Na kama tukitizama maana iliyo dhahiri ya aya hiyo itafahamika kwamba Kusai baina ya majabali hayo mawili sio dhambi, basi ibara hii inamaanisha kuruhusiwa Kusai katika Majabali mawili na wala haimaanishi uwajibikaji wa kusai katika Majabali hayo, katika hali ambayo inaeleweka wazi ya kwamba Kusai ni katika mambo yaliyo ya ulazima na ya wajibu katika Hijja, ama kama tukirejea katika sababu za kuteremshwa aya hiyo tutafahamu na kuelewa kwa uwazi kabisa ya kwamba ibara hiyo ni kwa ajili ya kuwaondolea watu shaka kuwa kutokufanya jambo hilo sio dhambi. Ama ni vizuri kama tutafafanuwa kwa undani kabisa kuhusu suala hilo.1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44 45 46 47 next