Saa za kazi
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

(KITABU MAFUNZO YA ELIMU YA QUR_ANI)

 

KUIELEWA NA KUIFAHAMU ELIMU YA QUR-ANI

Qur-ani ni kitabu kimoja wapo katika vitabu ambavyo Mwenyeezi Mungu ameviteremsha kutoka mbinguni, kitabu hicho toka pale mwanzo ambapo kimeteremshwa, mpaka sasa hivi kimesalimika na hakijaharibiwa, kimehifadhika na kitaendelea kuhifadhika.

Mada muhimu ambazo zimo katika kitabu hichi kitukufu ni kumjua Mwenyeezi Mungu na kumfahamu ili tuwe karibu naye, kisha kuyaelewa maneno ambayo ameyazungumza katika kitabu hicho.

Kabla hatujaingia katika mada muhimu, kwanza kabisa kuna ulazima wa kuifahamu Elimu ya Qur-ani, na vipi tutaweza kupambanua baina ya elimu ya Qur-ani na taf-siri ya Qur-ani, kwa hiyo katika mada hizi ni muhimu na ni vizuri tukaelewa maana ya maneno hayo.

Ufahamu wa kuitambua Qur-ani umegawika katika sehemu mbili:- nazo ni kama ifuatavyo:-

(a) Elimu zinazohusiana na Qur-ani, yaani elimu ambazo zinamsaidia mtu kuilewa zaidi Qur-ani.

(b) Elimu zilizokuwemo ndani ya Qur-ani.

Kwa ibara nyengine tunaweza tukasema hivi:

1. Sisi tunaingalia Qur-ani katika mitizamo miwili, kwanza kabisa tunaiangalia ni kama kitabu cha Mwenyeezi Mungu ambacho kuna uwezekano wa kukifanyia uchunguzi katika kuteremka kwake, na kimechukua muda gani katika kuteremka kwake au kimekusanywa vipi, na mengineyo yasiyokua haya, kama vile kupekua na kujiuliza je, kuna uhusiano baina ya Aya moja na nyengine ndani ya kitabu hichi au hakuna? Au kujiuliza, je hivi ndani ya kitabu hichi mna Aya ambazo zinazozichambua Aya nyengine? Au kufanya utafiti kuhusiana na Aya ambazo ni Naasikh na Aya ambazo ni Mansuukh n.k. Mtizamo huu basi ndio mtizamo ambao umebeba maana halisi ya neno (Ulumul- Qur-ani) lenye maana ya elimu zinazohusiana na Qur-ani, na huu ni mkusanyiko wa elimu tofauti, kama vile: elimu ya Tajuwidi, elimu ya Tafsiri, elimu ya Kisomo cha Qur-ani n.k.

2. Vilevile tuna mtizamo mwengine wa kuingalia Qur-ani, na mtizamo huu ni kule kukiangalia kitabu hichi kwa ajili ya kutaka kufaidika na mafunzo yaliomo ndani ya kitabu hichi na mtizamo huu unajulikana kwa jina la (Tafsiri ya Qur-ani), na tafsiri hutimia kwa kupitia mfumo maalum, moja kati ya elimu ambazo Mfasiri wa Qur-ani anatakiwa kuzielewa ni (Ulumul- Qur-ani).

Kwa maelezo ambayo tuliyoyaelezea hapo juu, itakua imeshaeleweka kua (Ulumul- Qur-ani) ndio hatua ya mwanzo kabisa ambayo mtu anatakiwa kuielewa, kabla hajaingia katika uwanja wa Tafsiri, kwa kutokana na siri hii basi, ndio maana mapema kabisa baada tu ya Mtume (s.a.w.w) kufariki, walijitokeza miongoni mwa Masahaba waliopiga hatua katika fani ya Qur-ani. Na kwa kutokana na kwamba Imamu Ali (a.s) ndiye mtu wa mwanzo aliye watangulia Masahaba wote katika kupiga hatua katika suala hili, ndio maana Jalalu Dini Suyutiy akasema: (mtu wa mwanzo miongoni mwa Makhalifa ambaye amepokea hadithi nyingi zaidi zinazohusiana na Qur-ani ni Ali bin Abii Taalib). Na baada ya Imamu Ali (a.s) wanafuatilia miongoni mwa Masahaba ni Abdullahi bin Abbaas, Abdullahi bin Masoud, na Ubayya bin Ka’ab, hawa ndio watu wenye daraja ya mwanzo katika fani hii ya Qur-ani.1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 next