BARUAKWA DADA
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

  JINA LA KITABU: BARUA KWA DADA

  MUANDISHI : MAHDI IDALATIYANI

KIMECHAPISHWA:NA TAASISI YA UTAMADUNI

CHAPA: YA KUMI NAMOJA

CHAPA: YA KWANZA MWAKA 1382

  MWAKA:1384.

KWA JINA LA MWENYEENZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UFAFANUZI WA MASUALA YANAYOHUSIANA NA UMUHIMU WA KUVAA HIJABU

Salamu alaikum dada mpendwa.

Barua yako ambayo umeniandikia nimeisoma.

Mimi suala la kuvaa hijabu kwa kumuiga mama yangu tu na bila ya kujua umuhimu wake silikubali, kwani sitaki niwe ni miongoni mwa wenye kuabudu mila zisizokua na msingi, sitaki kutolewa thamani, wala kua niko nyuma bali nataka niwe kama walivyo watu wengine katika jamii, mimi sitaki kutekeleza matakwa ya wazee bila ya kujua malengo yake, kwanza hasa nataka muniambie ni wapi Qur’ani imemtaka mwanamke avae hijabu? La pili ni kwa nini wanaume wawe huru na wawe wanatenda walitakalo, lakini wanawake wawe wamewekewa mipaka na vikwazo, na kwa nini hamutaki watu kuwawacha huru na kuyawachia mambo yaelekee kwa mtiririko wake wenyewe, kwani mkifanya hivyo mtaisalimisha jamii kutokana  na msuguano, nyinyi mmeifanya dini kua nzito na mambo mkayafanya magumu, mpaka mmefikia kumtaka mwanamke hata kama atakua yupo peke yake na akataka kusali basi ni lazima avae hijabu, hivi nyinyi mmemfanya Mungu kua ni mwanamme kiasi ya kwamba sisi tujistiri mbele yake? Nataka kujua hasa kutokuvaa kwangu hijabu kunamdhuru nani katika jamii? Mimi najipamba nitakavyo na ninavaa nguo nitakazo, mambo yangu mimi yanakuhusuni nini? Mimi sifanyi hivyo kwa ajili ya kuleta ufisadi, halafu ni kwa nini hamuwaambii wanaume wasiwaangalie wanawake bali mnatuambia sisi tuvae hijabu? Samahani msije mkanifikiria mimi kua sina dini au ni kafiri, amini usiamini mimi ni kama wewe namkubali Mwenyeezi Mungu na vile vile naikubali Qur’ani nami ni muumini wa kweli, na wala sitaki kukosa radhi za Mwenyeenzi Mungu, mimi sio miongoni mwa wale wasiojua fadhila, naelewa kuwa Mwenyeenzi Mungu amenipa neema chungu nzima, mimi niko katika bahari ya neema zake, na napenda kila siku nizidi kuwa karibu nae, na nimridhishe zaidi, na niwe muangalifu zaidi katika masuala tofauti, na niyaelewe undani wake masuala hayo, ili niishi katika njia iliyo sawa, na siyo niishi kama vile wanavyotaka watu, mimi nasema kwamba iwapo kuna watu chungu nzima wasiokuwa na hijabu basi kuvaa hijabu kwangu mimi kutakuwa na faida gani? Itakapokuwa kutokuvaa hijabu kwangu mimi kutasababisha watu kupotea basi tujaalie kwamba mimi nitavaa hijabu lakini kuna watu wangapi wasiovaa hijabu? Ambao bado watakuwa ni kizuizi na watakuwa ni sababu ya kuwapoteza watu, basi kuvaa au kutokuvaa hijabu kwangu mimi kuna tofauti gani? Ukiachia yote hayo lakini hebu nambieni hivi nyinyi ni kwa nini mnayafanya mambo kuwa ni magumu, na hata nywele moja ya mwanamke hamutaki ionekane, mimi nataka kuelewa nywele moja ina tatizo gani kuonekana, na italeta madhara gani, wewe ni lazima unipe mimi haki katika suala hili, na baadae nataka unieleze ni kitu gani kitakachonifanya mimi niwe na hijabu, na vipi mimi nitaweza kulikubali suala hili.

JAWABU

Kwa kweli barua yako nimeipata na imenifikia, na kusema kweli mwanzo nilikuwa sina shauku ya kukuandikia jawabu kuhusu masuala yako, lakini baadhi ya ibara zako zimenilazimisha mimi kukamata kalamu na kukujibu, ingawaje ni kwa ufupi kabisa, na ibara zenyewe zilizonisababisha

Kujibu ni hizi zifuatazo:

Mimi sitaki kufanya jambo nisilolijuwa malengo yake.

Mimi naikubali Kur-ani.

Mimi napenda Mwenyeenzi Mungu awe radhi nami.

Baada ya kuziona ibara hizi nikasema mwenyewe kwa mwenyewe:

Nitamuandikia ukweli ulivyo, itakapokuwa ni kweli anataka kuelewa ukweli ulivyo na iwapo ni kweli wewe unatafuta radhi za Mwenyeenzi Mungu basi utatoa muda wako kwa ajili ya kuyafikiria mambo haya, na utaitupia macho kur-ani, na pale utapoona.1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 next