Masomo ya kiislaam kitabu cha piliDeprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 MASOMO YA KI-SLAAM
KITABU CHA PILI![]() KABURI TUKUFU LA IMAM HUSEIN (A.S) HUKO KARBALA (IRAQ)
DIBAJI
Je, wajua nani Mwislamu? Mwislamu ni ambaye anaamini kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja na Muhammad ni Mtume wake wa mwisho. Kama ukiamini haya, basi wewe ni Mwislamu. Lakini haitoshi kusema tu kuwa mimi ni Mwislamu; bali ni wajibu juu yako kutenda kwa mujibu wa kanuni za Ki-islamu, ili uwe Mwislamu wa ukweli, na uishi duniani katika raha, na upate utukufu Akhera[1] kwa kuingia peponi na kupata ridhaa za Mwenyezi Mungu. Basi ni lazima juu yako kujitahidi kufanya hayo. Na Uislamu una sehemu tatu: (1) Asili (Mizizi) ya Dini (2) Matawi ya Dini (3) Tabia (Mwenendo) ya Dini Basi anayekubali kwa ukweli Asili ya Dini, na kutumia Matawi ya dini, na akiishajipamba na tabia ya dini, basi yeye ni mbora duniani na akhera (Kiyama [2]) Kitabu hiki kimesahihishwa na kimepangwa na Ayatullah Allamah Al-Haj Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Muasisi na Muhbiri Mkuu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania. Wabillahi Tawfiq
MASOMO YA KI-ISLAM
KITABU CHAPILI
1. Somo la Kwanza
Ndugu yangu,
|