Masomo ya kiislaam kitabu cha kwanza
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

 

MASOMO YA KI-ISLAMU

Kitabu cha Kwanza

KAABA TUKUFU , HUKO MAKKA

 

 

DIBAJI

Je, wajua nani Mwislamu?  Mwislamu ni ambaye anaamini kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja na Muhammad ni Mtume wake wa mwisho. Kama ukiamini haya, basi wewe ni Mwislamu.

Lakini haitoshi kusematu kuwa mimi ni Mwislamu; bali ni wajibu juu yako kutenda kwa mujibu wa kanuni za Ki-islamu, ili uwe Mwislamu wa ukweli, na uishi duniani katika raha, na upate utukufu Akhera [1] kwa kuingia peponi na kupata ridhaa za Mwenyezi Mungu.

Basi ni lazima juu yako kujitahidi kufanya hayo.

Na Uislamu una sehemu tatu:

(1) Asili (Mizizi) ya Dini

(2)Matawi  ya Dini

(3) Tabia (Mwenendo) ya Dini

Basi anayekubali  kwa   ukweli Asili   ya  Dini, na kutumia Matawi ya dini. na akiishajipamba na tabia ya dini, basi yeye ni mbora duniani na akhera (Kiyama [2])

Kitabu  hiki  Kimefasiriwa  na  Sheikh Muhammed Ali Ngongabure, na kimesahihishwa na kimepangwa na Ayatullah Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Muasisi na Muhubiri Mkuu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania.

Wabillahi Tawfiq.1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 next