Imam Mohammad TaqiDeprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 HISTORIA FUPI YA IMAM MOHAMMAD JAWAAD (A.S)
JINA LAKE NA NASABU YAKE (A.S). Jina lake tukufu ni Mohammad bin Ally bin Mussa bin Jaafar bin Mohammad bin Ally bin Hussein bin Ally bin abi Twalib (a.s). MAMA YAKE (A.S) Mama yake alikuwa ni mjakazi alie kuwa akiitwa Sakinah Marsiyya, na inasemekana ya kuwa alikuwa akitwa kwa jina la Khaziiran, na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo. KUNIA YAKE (A.S) 1- Abu Ally. 2- Abuu Jaafar. 3- vile vile huitwa kwa kuniya ya Abuu Jaafar Athani, ili kumtofautisha au kumpambanua na imam Baaqir (a.s). MAJINA YAKE MASHUHURI (A.S) 1- Al jawaad. 2- Attaqiyyu. 3- Az zakiiyyu. 3- Al qaaniu. 4- Al murtadhaa. 5- Al muntakhab, na mengineyo. TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S) Alizaliwa tarehe 10 mwezi wa Rajab mwaka 195 hijiria, na kuna kauli nyingine kuhusiana na kuzaliwa kwake tofauti na hii.
|