Abu Hurairah
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

Abu Hurairah Na Hadith ?

Kila kitu, baadaye kilikuja kupitia yeye. Baadhi ya sheria na itikadi za Dini, yote hayo yalikuja kupitia sentenso zake ambazo hazikuwa katika dini asili hapo mwanzoni. Je ni sentenso ngapi unazozidhania wewe kuwa ziliwatenganisha Wakristo kuacha uasili wao ?

  Yupo mtu mmoja aitwaye ABU HURAIRAH ambaye historia yake mimi nitaweleteeni hapo mbele baada ya punde. Mtu huyu anasema mwenyewe :

Amehadithia Abu Hurairah:
Hakuna Sahaba hata mmoja wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kama mimi ambaye amehadithia Hadith zaidi yangu isipokuwa 'Abdallah bin Amr (bin al-'As) ambaye alikuwa akiziandika ambapo mimi sikufanya hivyo.

Juzuu zote tisa za Sahih Bukhari zina Ahadith 7,068. Kati ya hizo kiasi cha Ahadith 1100 zimenakiliwa na mtu huyu, yaani tuseme katika maneno mengine kuwa yeye amenakili Ahadith kiasi cha 15.56% za Ahadith zote za Sahih Bukhari (kiasi cha 1/6).

(Hapa mbeleni nitawapatieni idadi sahihi za Ahadith alizozinakili Abu Hurairah katika Sahih Muslim).

Kama vile nilivyoonyesha juu ya "Abu Hurairah", yeye alijipinga mwenyewe na vile vile kisayansi. Hadith ifuatayo ni wazi ambapo yeye anainakili kwani inapingana na vile ‘Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na ‘Umm Salamah walivyoipokea. Iwapo sisi tutakubali kuwa ‘Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na ‘Umm Salamah walikuwa katika nyumba ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. wakati mwingi zaidi kuliko wake zake wengine, basi kwa urahisi tutambua pale penye tatizo.

Haya yapo katika ukurasa wa 81, katika sura:
Iwapo mtu aliye katika hali ya saumu akiamka asubuhi akiwa katika Janaba (je saumu yake itakuwa sahihi ?)

Hadith hii imetarjumiwa na mtarjumu tu hadi mwishoni mwa aya ya kwanza. Kufikia hapo, aliacha kutarjumu. Hata hivyo, bado ipo katika lugha ya Kiarabu. Kiasi kinachobakia ni tarjuma yangu. Iwapo wewe hautataka kuniamini, ninakushauri urejee katika maandishi ya Kiarabu. Zaid ya hayo, mimi nitakuletea vianzio zaidi kwa ajili ya kuelezea na tarjuma nilioyoifanya.

Amehadithia ‘Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na Umm Salamah:
“Baadhi za nyakati Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akiamka asubuhi huku akiwa katika hali ya janaba baada ya kujamiiana na wake zake. Yeye alikuwa akioga na kufunga saumu.

Imehadithiwa na Abu Bakr bin 'Abdur-Rahman : Mimi na baba yangu tulimwendea'Aisha naye akasema :
"Mimi ninatoa shuhuda kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. nyakati zingine alikuwa akiamka asubuhi akiwa katika hali ya Janaba kwa sababu ya kujamiiana, na wala si kutokwa manii usingizini na alikuwa akifunga saumu siku hiyo.” Kutoka hapo alimwendea Umm Salamah ambaye nae pia alihadithia hivyo hivyo.1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 next