Shia na Hadithi
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

Majibu Na Maelezo

Abdilahi Nassir

UTANGULIZI

Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimshukie bwana wetu na mwombezi wetu, Muhammad b. Abdillahi, na ali zake wema waliotakaswa wakatakasika, na wote wanaofuata nyayo zao.

Hiki ni kitabu cha pili katika mfululizo wa majibu yetu ya al-Khututul Aridhwa kilichoandikwa na marehemu Sheikh M. al-Khatib kwa lugha ya Kiarabu, kiasi cha miaka thelathini iliyopita, na kufasiriwa kwa Kiswahili huku Kenya, hivi karibuni, kwa jina la Misingi Mikubwa lliyojengewa Dini ya Ushia.

Katika kitabu hiki, tumejaribu kuyajadili yote yale ambayo Sheikh M. a(-Kbatib aliyaeleza dhidi ya Shia, kuhusu Hadith za Mtume Muhammad s.a.w.w. Na kama tulivyofanya katika kitabu chetu cha kwanza, Shia na Qur'ani, tumeyalinganisha hayo na yale yanayopatikana katika vitabu vya Kisunni.

Ni matumaini yetu kwamba, baada ya kukisoma kitabu hiki, itakudhihirikia kwamba hakuna hitilafu kubwa hivyo baina ya msimamo wa Sunni juu ya Hadith na ule wa ndugu zao, Shia, hata iwazuie wao kukurubiana na kuelewana kamaalivyopendelea Sheikh M. al-Khatib.   Kitu cha pekee kinachozuia ndugu wawili hao kuelewana ni zile chuki zinazojengwa baina yao na wale ambao watapata hasara lau ndugu hao watasikilizana na kulingana!

lli uweze kufaidika na majadiliano yaliyomo humu, na yale yaliyomo katika vitabu vyetu vingine katika mfululizo huu, ningependa uhakikishe kwamba:

(i)  unayo nakala ya hicho kitabu cha Sheikh M. al-Khatib tunachokijibu. Kama huna, jaribu kukipata kutoka mojawapo ya anwani hizi: S.L.P.70541; au 67971; au 48509: zote za Nairobi, Kenya.

Hivi vyetu, unaweza kuvipata kwa kutuandikia kwenyeS.L.P. 86260,     Mombasa, Kenya.

(ii) tunapotaja kwamba maneno fulani ya Sheikh M. al-Khatib yamo kwenye ukurasa fulani wa kitabu chake, hakikisha umefungua ukurasa huo na kuyakinisha kwamba tumeyanukuu maneno haya vilivyo.  Kamasivyo,

tafadhali tuandikie utukosoe ili tuweze kujisahihisha. Maana nia yetu si kumzulia marehemu S,heikh uwongo, bali ni kujenga umoja wa Waislamu kwa kujaribu kuondoa kutoelewana kulioko baina yao.

(iii) tunapotoa ushahidi wa vitabu fulani, ujaribu kuangalia ushahidi huo katika vitabu hivyo, kwa lugha unayoielewa. Kamahakuna kwa lugha hiyo, basi mwendee shekhe yeyote aliye karibu nawe, na ambaye hayuko upande wowote katika mzozo huu. umwombe akuangalilie katika nuskha za Kiarabu alizonazo yeye ili uhakikishe kwamba tulivyo nukuu ndivyo. Kama sivyo tafadhali usisite vile vile kutujulisha ili tuweze kuelekezana.1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 next