Hadithi ya KisaDeprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99 Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103 HADITHI YA SHUKA
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
KIMETARJUMIWA NA : SALIM NG’ANG’A MWEGA
DIBAJI
Kama vile yanavyobadilika yaliyomo ulimwenguni, vile vile maumbile ya binadamu hupatwa na mabadiliko. Tofauti zipatikanazo baina ya binadamu na binadamu mwingine husababisha tofauti pia katika tabia na nyenendo, kwa mfano katika unyenyekevu, kiburi, usahaulifu, kumbukumba nzuri, hisia ya kutaka hifadha, n.k. Kwa hivyo, ikiwa katika jamii baadhi ya itikadi, desturi na sheria, hazina misingi thabiti, na ikiwa watu wanaosimamia jamii hii sio waamimifu, bila shaka zitapatwa na mabadiliko na ulegevu, na hata mwishowe kutoweka kabisa. Hili ni jambo la hakika lililothibiti kwa njia ya uchunguzi na ujuzi. Ili kuepuka hatari hii na kuuhifadhi uislamu – Mtume Mtukufu (s.awa.) amesema ya kwamba: (اني تارك فيكم ما ان تمسكتم به لن تضلّوا بعدي احدهما اعظم من الآخر كتاب الله حبل ممدود من السماء الى الارض و عترتي اهل بيتي و لن يفترقا حتى يردا علي الحوض فانظروا كيف تخلفوني فيهما)[1] “Hakika mimi ninaacha kati yenu ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu, kimoja ni kitukufu kuliko cha pili navyo ni kitabu cha Mwenyezi Mungu (ambacho ni) kamba iliyonyooshwa toka binguni hadi ardhini na kizazi changu, (ambacho ni) Ahlu baiti wangu na wala havitatengana kamwe hadi vitakapo nikuta kwenye hodhi (ya kauthar). Basi angalieni vile mtakavyo vitendea baada yangu. (Sunanut Tirmidhi hadithi ya 3788.) 1) QURAN TUKUFU
Quran tukufu ndio chemchemi ya misingi na mafunzo ya kiislamu na uthibitisho wa kuwa kwake Kitabu cha Allah (ambacho ni muujiza) na pia ni uthibitisho wa utume wa Mtume Mtukufu wa uislamu. Quran tukufu ni neno la Allah, lililofunuliwa kwa Mtukufu Mtume(s.awa.) na kwa kupitia kwake liliwafikia wanadamu. Quran tukufu inawapa wanadamu ujuzi wa kielimu na kivitendo, ambao kwa kuutumia ipasavyo, binadamu anaweza kufanikiwa kuchuma mema, amani na mafanikio humu duniani na huko akhera. Lengo hasa la Quran tukufu ni kuwaongoza wanadamu ili kupata maendeleo na mafanikio. Inawapa wanadamu elimu kwa njia nzuri, nyepesi na ya dhahiri, kuhusiana na itikadi zilizo sahihi, tabia njema na matendo mema ambayo ni muhimu sana katika maisha ya kila mmoja, na vile vile katika maisha ya jamii. Allah (S.B.) amesema katika Quran tukufu. ((ونزّلنا عليك الكتاب تبياناً لكل شيء و هدىً و رحمة و بشرى للمسلمين))
|