Hadithi za mtume
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

Kimetarjumiwa Na:Ductoor A Kadiri

Kwa jina Ia Mwenyezi Mungu. Mwingi warehema. Mwenye kurehemu.

Sifa zote ni kwa Mwenyezi Mungu Aliyetuokoa na ujahiliya wa zamani. Tunamwomba Atujaalie pia kuutupilia mbali ujahiliya wa kileo. Tuwe ni wenye kufwata barabara maagizo Yake na mafundisho ya Mtume Wake S.A.W. na tuwe ni katika umati bora uliowahi kutokea kwa watu.

Umma wetu wa Kiislamu, kwa kipindi sasa umenyonyorwa mengi: akili, fikra na hata mapato na mwisho kuachiwa mizozo na utengano na kutusahaulisha wajibu wetu. Hivyo, jinsi ya kujua namna ya kujirudishia haki zetu ni kurudi kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Kurani Tukufu) na kwenye mafunzo ya Mtume Wake S.A.W. ambaye ni kiigizo chema kwetu sisi. Kwake yeye ndiko tutapata ufanisi wetu wa mambo yote: uongofu wa akili, malezi ya kiroho, maelekezo ya kiibada, kijamii, kisiasa, kiuchumi na shifaa ya yaliyo nyoyoni.

Kitabu hiki ni mkusanyiko wa baadhi ya mafunzo yake S.A.W. ambayo yanatupa msingi  wa yote hayo, kimetarjumiwa kwa Kiswahili kutoka kile cha Kiarabu kilichotolewa kwa mara ya kwanza hapo mwaka 1982 na DAR EL TAWHEED ya huko Tehran, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Tunatumai Inshaallah kitakuwa na manufaa kwa sote. Na pia tunataraji kitafaa katika madrassa zetu za Kiislamu huku Afrika Mashariki na hasa kwa watumiao lugha yetu ya Kiswahili.

Na mwisho, tunamshukuru sana Sheikh Abdillahi Nassir kwa kukubali kupoteza masaa yake mengi kupitia mswada wa tarjuma hii na vile vile kwa ushauri wake alio­tupa. Mwenyezi Mungu Amjazi heri.

Taasisi ya Fikra za Kiislamu,

Tehran,

Jamhuri ye KiisIamu ye Iran.

Alisema Mtume Muhammad (SAW):

Aliye mbali mno kufanana nami kati yenu ni bahili, mchafu, mwenye mambo ya aibu.1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 next