Al-Sahifat Al –kamilat Al-Sajjadiyya
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

Kimeandikwa na: Ali ibn al - Husayn Imam Zaynul al - Abidin (a.s.)

Kimetafsiriwa na: Sheikh Haroon Pingili

® Haki ya kunakili imehifadhiwa na: Bilal Muslim Mission of Tanzania

Shukrani

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.

Tunamshukuru Allah (s.w.t.) na baraka za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul ~ Bayt (a.s.) kwa kutujaalia kuweza kufanikia juhudi zetu hizi katika kuchapisha kitabu hiki "Sahifatul Kamillah Al-Sajadia".

Kitabu kilochopo mikononi mwako ni tafsiri ya kitabu cha Kiarabu, kiitwacho "As-Sahifatul Kamillah Al-Sajadia" kilichoandikwa na Imamu wa Nne Al-Imam Zainul Abdeen (a.s.). Ndani ya Kitabu hiki Imam (a.s.) ameelezea Du'a mbali-mbali.

Sababu iliyoifanya Mission yetu isimamie kazi hii ni kama zile za mwanzo, ambayo zinatokana na maombi ya Maulamaa wengi katika Afrika Mashariki kututaka tukifanyie tarjuma kitabu hiki kiingie kwenye lugha ya Kiswahili.

Tunamshukuru Shaikh Harun Pingili kwa kutukubalia ombi letu na kuifanya kazi hii kwa moyo mmoja, na vile vile Bilal Muslim Mission of Scandinavia kutukubalia kukichapisha kitabu hiki.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tena kwani vitabu vyetu vya mwanzo vimependwa mno na wasomaji na hivyo kutupa ari ya kuchapisha hiki ulichonacho mkononi na kitakachofuatia Insha-Allah.

Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa wale wote ambao kwa juhudi zao kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi na waliosaidia kwa njia moja au nyingine katika tarjuma na uchapishaji wa kitabu hiki. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) awalipe malipo mema hapo Duniani na baadaye huko, Akhera.1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44 45 46 47 48 49 50 51 52 53 54 55 56 57 58 59 60 61 62 63 64 65 66 67 68 69 70 71 72 73 74 75 76 77 78 next