Dua Iliyokubaliwa
Deprecated: Function eregi_replace() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 99

Deprecated: Function split() is deprecated in /home/swaalshia/public_html/page.php on line 103

 

"Ewe Mola! Usinirejeshe nyumbani kwangu!"

Haya ni maneno aliyoyasikia Hind, mke wa Amru bin Jumuuh, kutoka kwa mume wake alipokuwa akiondoka nyumbani baada ya kujiandaa kwa silaha kwenda kushiriki katika vita vya Uhud. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Amru bin Jumuuh kushiriki katika jihadi pamoja na Waislamu wengine. Hajawahi kabla yake kupigana vita kwa sababu alikuwa na kilema cha mguu ambao ulikuwa ukichechemea sana. Kufuatana na hukumu wazi wazi ya Qur'ani Tukufu, jihadi si wajibu kwa kipofu, kiwete na mgonjwa. Ingawa yeye mwenyewe hajawahi kushiriki katika jihadi, lakini alikuwa na wanawe wanne kama simba ambao daima walikuwa pamoja na Mtume Muhammad (SAW) katika medani za vita.

Hakuna mtu aliyefikiria kwamba Amru, juu ya kuwa na udhuru wake na baada ya kuwapeleka wanawe wanne katika jihadi, angetaka yeye mwenyewe awe miongoni mwa askari wa Kiislamu.

Jamaa zake waliposikia juu ya uamuzi wake, wakamwendea kutaka kumshawishi abadilishe uamuzi wake.

"Kwanza kabisa, kwa mujibu wa sheria, wewe umesamehewa usipigane jihadi. Pili, una watoto wanne mashujaa ambao wamekwenda pamoja na Mtume Mtukufu vitani. Kwa hivyo, hakuna haja yo yote ya kujiunga katika jeshi."1 2 3 4 5 next